#Football #Sports

KIVUMBI UCL: REAL MADRID v BAYERN, SPORTING v ARSENAL

Ligi kuu ya Mabingwa barani Ulaya inarejea kwa kishindo huku mechi mbili zikichezwa usiku wa Leo. Real Madrid watakua uwanjani Santiago Bernebeau kupambana na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika mchezo wa kukata na shoka unaosubiriwa na mashabiki Wengi duniani. Bayern hawana rekodi nzuri dhidi ya Madrid na hivyo watakua wakiangazia kuiweka rekodi hiyo nyuma.

Katika mchezo mwingine, Sporting Lisbon ya ureno watawaalika vijana wa Mikel Arteta Arsenal, huku Arsenal wakiwa wamepoteza michezo miwili waliyocheza hivi karibuni. Ni matokeo yanawapa motisha na kujiamini Sporting lakini Arsenal watakua wakiangazia kuendeleza rekodi ya kutoshindwa kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Michuano hiyo itaanza mwendo wa saa nne usiku.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *