#Local News

MURKOMEN, KANJA KUFIKA BUNGENI KUHUSU UHUNI

Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, na inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, wameagizwa kufika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu utawala na usalama Jumanne wiki ijayo kuhusiana na ongezeko la uhuni na ujambazi nchini.

Maagizo hayo yaliyotolewa na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, yanajiri huku wabunge wakiibua hofu kuhusiana na kuzorota kwa usalama kunakochangiwa na vurugu zinazoonekana kuchochewa kisiasa.

Kamati hiyo inatarajiwa kumshinikiza Murkomen kuweka wazi mikakati iliyowekwa kudhibiti makundi ya wahuni yanayoendelea kuchipuka nchini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *