MUYOTI ASIFU USHINDI WA KENYA POLICE DHIDI YA AFC LEOPARDS
Kocha mkuu wa Kenya Police Nicholas Muyoti amesema ushindi wao wa mabao matatu kwa bila dhidi ya AFC Leopards umetokana na mpango madhubuti wa kiufundi uliotekelezwa vizuri na wachezaji wake
Muyoti amesema kuelewa mbinu za mpinzani pamoja na nidhamu ya kikosi chake uwanjani kulichangia sana kupata alama zote tatu huku akiwataka washambuliaji wake kuendelea kuwa makini mbele ya lango katika mechi zijazo
Kwa upande wake kocha wa AFC Leopards Fred Ambani amesema makosa ya safu ya ulinzi ndiyo yaliwagharimu pakubwa katika kipigo hicho akiwahimiza wachezaji wake kuimarika na kuonyesha ustahimilivu katika michezo inayofuata.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































