‘TUWEKE WAKENYA MBELE KWA KUPINGA MSWADA WA 2024-2025’ ASEMA MUGABE
Mbunge wa Likuyani Innocent Mugabe amewataka wabunge kusimama na wananchi na kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024-2025 kwa madai kwamba wabunge wengi huwa wanawatelekeza wapiga kura
Akiwa katika eneo bunge la Lwanda kaunti ya Vihiga Mugabe amesema tayari wakenya wanaendelea kuteseka kutokana na mswada wa kifedha 2023 ambao uligeuka kuwa sheria na mzigo huo haufai kuongezwa kwa wakenya
Mugabe vile vile ameongeza kuwa wabunge wengi usahau wakenya pindi tu wanapochukua nyadhifa za uongozi na kuwataka kuweka kipaumbele maslahi ya wakenya kwa kukataa watozwe zaidi kodi hasa wakatu huu wanaendela kusakamwa na hali ngumu ya Maisha.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































