MVUTANO WAZUKA NDANI YA BARAZA LA MAWAZIRI
Mvutano wa kisiasa unaendelea kushuhudiwa ndani ya Baraza la Mawaziri la Rais William Ruto, huku mawaziri wakionekana kuchukua misimamo tofauti kufuatia matamshi yenye utata yanayodaiwa kutolewa na Waziri wa Afya, Aden Duale.
Ripoti zinaonyesha kuwa baadhi ya mawaziri wameonyesha kutofautiana kwa kauli na misimamo kuhusu suala hilo, hali inayozua maswali kuhusu mshikamano ndani ya serikali.
Wakati huo huo, mjadala kuhusu urithi wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 unaendelea kushika kasi, huku Naibu Rais Kithure Kindiki akitajwa kuwa chini ya shinikizo kutokana na ushindani wa kisiasa unaoibuka.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































