MGOMO WA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WASITISHWA
Ni afueni kwa wasafiri wanaotumia ndege baada ya Wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kusitisha mgomo uliokuwa umepangwa baada ya kusaini makubaliano ya awali na waajiri katika sekta hiyo.
Makubaliano hayo yanakuja siku chache baada ya Muungano wa KAWU kutangaza mgomo huku pande zote zikikubaliana kuanza mazungumzo kuhusu masuala ambayo bado hayajapatiwa suluhu.
Mazungumzo hayo yatalenga kushughulikia malipo ya mishahara, usalama wa ajira na kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































