#Local News

RUKU: SIFUNA BADO SI TISHIO KWA RUTO 2027

Huku mchakato wa mimi ndio sifuna ukishika kasi katika anga za kisiasa, Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, amesema Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, bado hajafikia kiwango cha kuwa mpinzani mkubwa wa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Akizungumza katika mahojiano na runinga moja humu nchini , Ruku amekiri kuwa umaarufu wa Sifuna unaendelea kuongezeka, lakini akasisitiza kuwa hali hiyo haimuweki miongoni mwa viongozi wakuu wanaowania urais nchini.

Aidha, amesema Rais Ruto anaendelea kuwa na msingi imara wa kisiasa, akieleza kuwa ushindani wa mwaka 2027 utaamuliwa na uwezo wa wagombea kujenga uungwaji mkono wa kitaifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *