RUKU: SERIKALI INAHITAJI SHILINGI BILIONI 10 KUKABILI UHABA WA CHAKULA
Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, amesema serikali inahitaji takriban shilingi bilioni 10 ili kusaidia wananchi wanaokabiliwa na athari za uhaba wa chakula.
Ruku amesema fedha hizo hazijatengwa katika bajeti ya sasa, hali ambayo imeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa serikali katika juhudi za kudhibiti athari za kupanda kwa bei ya vyakula.
Aidha, amesema matumizi ya fedha za ziada kugharamia mipango ya kupunguza gharama za chakula yanaongeza mzigo kwa uchumi wa nchi, licha ya umuhimu wake katika kuwakinga wananchi dhidi ya mfumuko wa bei.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































