VIPERS SC YAICHAPA GOR MAHIA 1 – 0 DAKIKA ZA MWISHO
Vipers SC ya Uganda imeichapa Gor Mahia bao 1-0 katika mechi ya Kundi A ya Mashindano ya CECAFA Kagame Cup iliyochezwa mjini Kigali, Rwanda.
Gusto Mulongo aliifungia Vipers SC bao la ushindi katika dakika za nyongeza baada ya kuunganisha mpira wa kichwa uliomshinda kipa wa Gor Mahia, Humphrey Katasi.
Kocha Charles Akonnor alifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi cha kwanza kilichoifunga APR mabao 5-0, akiwapa nafasi ya kuanza wachezaji kadhaa wapya, wakiwemo Hansel Ochieng’, Ebenezer Adukwaw na Ben Stanley Omondi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































