AFC LEOPARDS WAMTEUA BERNARD MWALALA KAMA KOCHA MSAIDIZI
AFC Leopards wamemteua Bernard Mwalala kuwa kocha msaidizi wa kwanza wa klabu hiyo, wakilenga kuimarisha benchi la ufundi kuelekea msimu mpya.
Mwalala anajiunga na AFC Leopards akitokea Bandari, ambako alikuwa akihudumu kama kocha mkuu.
Uongozi wa AFC Leopards unasema uteuzi wa Mwalala utaimarisha kikosi na kuongeza nafasi ya klabu hiyo kupigania mataji katika msimu ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































