WANZA AINYAKULIA KENYA FEDHA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA
Diana Wanza ameinyakulia Kenya medali ya fedha katika mbio za wanawake za mita 10,000 kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 mjini Glasgow, huku bingwa wa dunia Lilian Odira akifuzu kwa urahisi nusu fainali ya mbio za mita 800.
Wanza alimaliza mbio hizo kwa muda wa dakika 31:50.13, akishika nafasi ya pili nyuma ya Rose Davies wa Australia, aliyeshinda medali ya dhahabu kwa muda wa dakika 31:39.32.
Medali hiyo imeiongezea Kenya medali ya pili katika mashindano hayo, huku taifa likiendelea kusubiri kutwaa tena dhahabu ya mbio za wanawake za mita 10,000, baada ya ushindi wa Joyce Chepkirui mwaka 2014.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































