DCI YACHUNGUZA VURUGU ZA MBALE
Idara ya upelelezi wa jinai DCI imeanzisha uchunguzi katika tukio la vurugu baina ya makundi mawili hasimu zilizoshuhudiwa mjini Mbale kaunti ya Vihiga wakati wa mkutano ulioongozwa na katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna, na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyetambuliwa kama George Otobe, mkazi wa Kisumu.
Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa Otobe alimdunga mtu mmoja kisu kichwani awali kutokana na tofauti za kisiasa, na hivyo kusababisha waliokuwa karibu kulipiza kisasi, DCI ikiwataka wanasiasa kuhakikisha wafuasi wao hawabebi salaha kwenye mikutano.
Haya yanajiri huku upinzani ukikana madai ya kupanga vurugu kwenye mikutano yao.\
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































