#Local News

MAAFISA WA NAIROBI HOSPITAL MAHAKAMANI

Maafisa kadhaa wa Nairobi Hospital wamefikishwa katika mahakama ya Milimani baada ya kukamatwa katika njia tatanishi kuhusiana na makosa ambayo hayajawekwa wazi.

Maafisa hao ni mshauri wa matibabu ya wanawake Dakta Job Obwaka, naibu mwenyekiti wa bodi ya hospitali hiyo Samson Kinyanjui, mkurugenzi Valery Gaya na mkurugenzi wa zamani Chris Bichage.

Kukamatwa kwao kumekosolewa na mawakili na usimamizi wa muungano wa madaktari, KMPDU.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *