#Local News

WAWILI WAKWAMA JENGONI WESTLANDS

Shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo la Westlands jijini Nairobi kuwakoa wafanyakazi wawili waliokwama baada ya sehemu ya jengo la ghorofa 22 kuporomoka usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa shirika la msaada la Kenya Red Cross, wafanyakazi wawili waliokolewa bila majereha, na kuongeza kuwa hali ya waliokwama bado haijulikani.

Mkasa huo unajiri siku 2 baada ya watu wengine 4 kufariki kwenye mkasa sawa katika eneo la Blue Estate mtaani Shauri Moyo, jijini Nairobi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *