#Local News

WAATHIRIWA WA MAANDAMANO WATHIBITISHWA

Jumla ya waathiriwa 1,800 wamethibitishwa kuathirika na ukiukaji wa haki za kibinadamu wakati wa maandamano, orodha ya waathiriwa hao ikiratibiwa kuwasilishwa kwa Rais William Ruto kabla ya mchakato wa fidia kuanza.

Tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu, KNCHR, imethibitisha malalamishi ya waathiriwa hao, na kupendekeza fidia ya shilingi milioni 3 kwa waliouawa na shilingi milioni 4 kwa waathiriwa wa dhuluma za kijinsia.

Kulingana na mwenyekiti wa tume hiyo Claris Ogangah, mbali na fidia ya fedha, waathiriwa pia watapokea matibabu, ushauri nasaha na mageuzi katika idara ya usalama kuhusu kushughulikia maandamano.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAATHIRIWA WA MAANDAMANO WATHIBITISHWA

UHABA WA MBOLEA WAZUA HOFU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *