#Football #Sports

VIPERS SC YAICHAPA GOR MAHIA 1 – 0 DAKIKA ZA MWISHO

Vipers SC ya Uganda imeichapa Gor Mahia bao 1-0 katika mechi ya Kundi A ya Mashindano ya CECAFA Kagame Cup iliyochezwa mjini Kigali, Rwanda.

Gusto Mulongo aliifungia Vipers SC bao la ushindi katika dakika za nyongeza baada ya kuunganisha mpira wa kichwa uliomshinda kipa wa Gor Mahia, Humphrey Katasi.

Kocha Charles Akonnor alifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi cha kwanza kilichoifunga APR mabao 5-0, akiwapa nafasi ya kuanza wachezaji kadhaa wapya, wakiwemo Hansel Ochieng’, Ebenezer Adukwaw na Ben Stanley Omondi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *