RAIS WILLIAM RUTO APIGIWA DEBE UKAMBANI
Siasa za kumpigia debe Rais William Ruto zimeendelea kushika kasi katika eneo la Ukambani huku viongozi wanaounga mkono serikali wakiongeza juhudi za kuimarisha uungwaji mkono wa utawala wa Kenya Kwanza.
Viongozi hao wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara na kushirikiana na wananchi katika maeneo mbalimbali ya Ukambani wakisisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, huduma za afya na kuboresha sekta ya kilimo.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































