KENNEDY KALOMBOTOLE AFIKISHWA MAHAKAMANI
Mwanamume anayekabiliwa na mashtaka ya kumuua mgonjwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta Kennedy Kalombotole amefikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la mauaji baada ya kucheleweshwa kwa kesi yake kwa miezi kadhaa
Kalombotole alifikishwa mbele ya Jaji Diana Kavedza katika Mahakama Kuu jijini Nairobi ambapo alikana shtaka la mauaji.
Kesi hiyo ilikuwa imesubiri kukamilika kwa uchunguzi wa kubaini iwapo alikuwa na uwezo wa kiakili wa kujibu mashtaka yanayomkabili.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































