WANAFUNZI MARSABIT WAENDELEA KUTIBIWA KUFUATIA ‘KICHAPO’
Wizara ya elimu imeanzisha uchunguzi katika kisa cha kusikitisha ambapo wanafunzi 36 wa shule ya upili ya wasichana ya Maikoma kaunti ya Marsabit wanadaiwa kupewa adhabu kali na walimu baada ya wanafunzi hao kulalamika kwamba walishinda na njaa wakati wa tamasha za muziki.
Kulingana na picha ambazo zimeibua shutuma, wanafunzi hao wanaonekana wakiwa na alama za kupigwa migongoni na miguuni, ikiripotiwa kwamba walipigwa kwa kebo za mtambo wa banseni unaotumika katika maabara.
Katibu mkuu katika idara ya elimu ya msingi Dakta Julius Bitok amesema uchunguzi unaendelezwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































