RAIS FAYE ATANGAZA HOLIDEI SENEGAL KUSHEREHEKEA AFCON
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, ametangaza siku ya mapumziko nchini humo hii leo ili kuwapisha wananchi kusherehekea ubingwa wa dimba la taifa bingwa barani Afrika, AFCON, walilotwaa hapo jana nchini Morocco.
Katika tangazo, rais Faye amesema holidei hiyo inalenga kuwawezesha raia kushiriki sherehe za alichokitaja kama fahari kuu ya taifa.
Kupitia runinga ya kitaifa ya RTS baada ya ushindi wa simba hao wa Teranga, Faye amewahimiza raia kuadhimisha sherehe hizo kwa umoja na hadhi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































