HUDUMA ZA AFYA ZATATIZIKA HOSPITALI YA MAMA LUCY
Huduma za afya katika hospitali ya mama Lucy katika kaunti ya Nairobi zimetatizika kufuatia mgomo wa matabibu na madaktari wa Kaunti huku madaktari wanafunzi wakiachwa kushughulikia Wagonjwa.
Chama cha matabibu nchini kimesisitiza kuwa wanachama wake hawatarudi kazini hadi pale madai yao yatakaposikilizwa na Serikali ambayo ni Pamoja na kulipwa kwa malimbikizi ya mishahara ya miezi kumi na tisa.
Chama hicho kimeitwa kwa mkutano na baraza la magavana ili kuweza kutafuta suluhu kwa Mgomo huo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































