#Local News

FAMILIA YATAKA HAKI KUFUATIA KIFO CHA ALPHY MIGASHA

Familia ya Alphy Migasha inataka kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani kwa afisa wa kijeshi anayeshukiwa kumuua ndugu yao baada ya kumpiga kikatili katika mtaa wa Umoja One, jijini Nairobi.

Haya yanajiri huku ripoti ya uchunguzi wa maiti ikibainisha kuwa Alphy alifariki kutokana na gando la damu kwenye mapafu liliLOtokana na majeraha aliyoyapata marehemu wakati wa shambulizi hilo, ambapo mguu wake ulivunjika kufuatia kupigwa na mshukiwa.

Familia hiyo imewaomba makachero wa kitengo cha mauaji, ambao wamechukua jukumu la uchunguzi, kuhakikisha haki inapatikana kwa kifo walichokitaja kuwa cha mapema na chenye uchungu, wakisema marehemu alikuwa nguzo ya familia.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *