ROSENIOR APUUZILIA MBALI TETESI ZA COLE PALMER KUJIUNGA NAMANCHESTER UNITED
Kocha wa Chelsea Liam Rosenior amepuuzilia mbali madai ya Cole
Palmer kuondoka Stamford Bridge, akisema hatua hiyo ni
isiyowezekana licha ya ripoti zinazomhusisha na uhamisho kwenda
Manchester United.
Palmer, mzaliwa wa Manchester, alijiunga na Chelsea kutoka
Manchester City mwaka 2023 na haraka akajitokeza kama mchezaji
muhimu wa klabu hiyo katika misimu yake miwili ya kwanza jijini
London.
Ripoti zimeibuka zikidai mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23
anaweza kuwa na nia ya kurejea kaskazini mwa England na kujiunga
na klabu aliyokuwa akiishabikia akiwa mtoto.
Hata hivyo, mchango wa Palmer msimu huu umeathiriwa na majeraha
ya mara kwa mara, akifunga mabao matano bila kutoa pasi ya bao
katika mechi 13 alizocheza kwenye mashindano yote.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































