#Local News

OSORO AWAAMBIA UPINZANI KULETA AJENDA KABLA YA IEBC

Mbunge wa South MugirangoSylvanus Osoro, amewatilia shaka wanasiasa wa upinzani, akiwashauri kuweka wazi ajenda yao ya kile wanachokusudia kufanya kwa wananchi kabla ya kufika Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuzungumzia maandalizi ya uchaguzi.

Akizungumza katika sherehe iliyofanyika Kaunti ya Kisii chini ya uongozi wa Rais William Ruto, Osoro alidai kuwa wanachama wa United Opposition hawana ajenda thabiti.

Osoro amewataka kwanza kukubaliana juu ya mgombea urais, kuwa na ajenda ya wazi, kisha waende IEBC kuwasilisha masuala yao kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027, akisisitiza umuhimu wa uwazi na maandalizi ya kweli.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *