BUNGE LAIMARISHA UANGALIZI WA HAZINA MPYA
Bunge limewaondolea wakenya hofu ya fedha za hazina mpya ya miundombinu kufujwa kutokana na muundo wake wa awali, baada ya kuidhinisha kubuniwa kwa baraza litakalosimamia hazina hiyo.
Kwa mujibu wa mswada wa hazina hiyo, baraza hilo litamjumuisha Waziri wa fedha, gavana wa Benki Kuu ya Kenya, mwanasheria mkuu wa serikali, na wanachama wengine 6 wasio watumishi wa umma.
Miongoni mwa majukumu yake ni kuelekeza na kuishauri bodi ya hazina hiyo, huku bunge likijipa mamlaka ya kuidhinisha sera ya uwekezaji wa hazina hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































