#Local News

LINDA MWANANCHI YATAKA POLISI WALIOWAVURUGA KUKAMATWA

Viongozi wa chama cha ODM wanaoegemea mrengo wa Linda Mwannchi, wametaka hatua mwafaka kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa polisi waliowarushia viongozi hao vitoza machozi na kuvuruga mkutano wao mjini Narok hapo jana.

Wakiongozwa na seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, mwenzake wa Vihiga Godfrey Osotsi, gavana wa Siaya James Orengo, na mbunge wa Embakasi East Babu Owino, viongozi hao wamewashutumu polisi kwa madai ya kuendelea kuwahangaisha, hatua wanayoitaja kuwa ukiukaji wa haki za kidemokrasia.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *