MAGAVANA WATAKA ONGEZEKO LA MGAO WA KAUNTI
Baraza la Magavana limetaka mgao wa shilingi bilioni 534 katika mwaka ujao wa kifedha, likisema kaunti zinahitaji fedha zaidi kulipa wafanyakazi na kutekeleza majukumu yao.
Mwenyekiti wa baraza hilo, Ahmed Abdulahi, ameeleza kuwa mahitaji ya kaunti yameongezeka na yanahitaji kuzingatiwa katika upangaji wa bajeti.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Ugavi wa Rasilimali, Mary Chebukati, amependekeza mgao wa shilingi bilioni 458.9 kwa mwaka wa kifedha wa 2026/2027, akisema matumizi ya kaunti yameongezeka huku zikipokea shilingi bilioni 415 katika mwaka huu wa kifedha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































