KINDIKI ATOA UJUMBE WA UMOJA WANAPOADHIMISHA PASAKA
Naibu Rais, Kithure Kindiki, amewahimiza Wakenya kujitafakari, kudumisha umoja na kujirekebisha wakati wa kipindi cha Pasaka, akieleza kuwa kujitoa kwa Yesu Kristo ni kielelezo cha hali ya juu cha upendo.
Katika ujumbe wa Ijumaa Kuu, Kindiki amesema Pasaka inaonyesha mfano mkubwa zaidi wa upendo kuwahi kushuhudiwa, akisisitiza umuhimu wa kipindi hicho katika kalenda ya Wakristo.
Ameongeza kuwa Pasaka ni fursa ya matumaini na ukombozi, akibainisha kuwa ni kipindi muhimu katika safari ya kiroho ya waumini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































