WAKENYA WALAZIMIKA KUHONGA KUHUDUMIWA- RIPOTI
Imebainika kwamba upatikanaji wa huduma hapa nchini unategemea uwezo wa mtu kutoa hongo kwa walio katika nafasi za kutoa huduma za kimsingi kama vile vitambulisho, pasipoti za usafiri na ajira.
Kwenye ripoti yake mpya ya mwaka 2025, tume ya maadili na kukabili ufisadi, EACC, imesema hongo hutumika kuharakisha utoaji wa huduma, kuepuka faini au kupata huduma zinazopaswa kutolewa bila malipo.
Maafisa wa polisi, usajili wa kiraia na usafiri ndio wametajwa pakubwa kuhusika na ufisadi, EACC ikiwahimiza wakenya kutoa taarifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































