SAKAJA AKABILIWA NA HATARI YA KUKAMATWA BAADA YA KUPUUZA WITO WA SENETI
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja anakabiliwa na uwezekano wa kukamatwa baada ya kushindwa kwa mara ya pili kufika mbele ya kamati ya Seneti inayochunguza madai ya uhamishaji haramu wa wakazi katika eneo la Old Ngara
Maseneta walikuwa wamemwita gavana huyo kujibu maswali kuhusu kuondolewa kwa wapangaji kupisha mpango wa nyumba za gharama nafuu lakini hakujitokeza katika kikao cha Alhamisi asubuhi
Kamati ya Seneti ya Haki Sheria na Haki za Kibinadamu sasa imetoa wito wa mwisho ikimtaka Sakaja kufika Mei saba mwaka elfu mbili ishirini na sita takriban miezi saba tangu suala hilo kuibuliwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































