#Football #Sports

NAIROBI UNITED WAKUTANA NA KCB ROBO FAINALI YA FKF CUP

Mabingwa watetezi Nairobi United wataongoza ratiba ya robo fainali ya kombe la FKF baada ya kupangwa dhidi ya KCB  katika droo iliyofanyika hii leo

Hafla ya upangaji ratiba iliwashirikisha magwiji wa soka la Kenya akiwemo mshambuliaji wa zamani wa AFC Leopards Daktari JJ Masiga pamoja na aliyekuwa nyota wa Gor Mahia Peter Dawo walioongoza shughuli hiyo

Nairobi United wamekuwa katika kiwango bora kwenye mashindano hayo wakitinga hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Posta Rangers hatua ya kumi na sita bora kufuatia ushindi mkubwa wa mabao nane kwa sufuri dhidi ya BMC Allstars katika mechi za awali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *