GEN-Z KAKAMEGA WAKATAA MAZUNGUMZO NA GAVANA WAO
Vijana wa kizazi cha Gen-Z katika kaunti ya Kakamega wamepuuzilia mbali uwezekano wa kuwapo kwa mazungumzo baina yao na gavana wa kaunti hiyo Fernandez Baraza.
Vijana hao wanasema kuwa ,gavana Baraza anapaswa kutekeleza malalamishi waliyowasilisha kwake badala ya kuitisha vikao kwa kuwa kulingana nao hawatashiriki mazungumzo na kwamba watakaofanya hivyo watakuwa wasaliti wa vijana wenzao.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 






























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































