#Local News

SONKO AONYA UPINZANI DHIDI YA MGAWANYIKO

Wakati viongozi wa upinzani wakizidi kuonyesha nia ya kuwania urais mwaka 2027, hofu inaongezeka kwamba mgawanyiko unaweza kudhoofisha uwezo wao wa kushindana dhidi ya Rais William Ruto.

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko ameonya viongozi wa upinzani kuwa wanapaswa kuungana nyuma ya mgombea mmoja wa urais ili kuongeza nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu.

Sonko amesema kuwasimamisha wagombea wengi kutagawanya kura za upinzani na kumpa Rais William Ruto nafasi kubwa ya kutetea kiti chake kwa muhula wa pili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *