SABINA CHEGE ATETEA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YA MATOKEO YA UCHAGUZI
Mjadala umezuka baada ya Tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC kutoa pendekezo la kusitisha zoezi kuwasilisha matokeo ya uchaguzi ya moja kwa moja.
Mbunge Mteule Sabina Chege amesema IEBC haijatoa sababu za kuridhisha za kusitisha matangazo au matokeo ya moja kwa moja ya matokeo ya uchaguzi.
Sabina Chege amesema zoezi hilo huwafahamisha Wakenya kuhusu mwenendo wa uchaguzi, huimarisha uwazi na husaidia kupunguza taharuki badala ya kuzua sintofahamu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































