IEBC YAENDESHA USHIRIKISHWAJI WA UMMA KUHUSU UFADHILI WA KAMPENI
Maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 yanaendelea kushika kasi, huku juhudi zikiongezwa kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakuwa wa haki, uwazi na unaoaminika kwa wananchi wote.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inaendesha vikao vya ushirikishwaji wa umma kote nchini ili kukusanya maoni kuhusu kanuni zinazopendekezwa za ufadhili wa kampeni za kisiasa.
IEBC imesema kanuni hizo zinalenga kuimarisha uwazi na usawa katika kampeni za kisiasa, huku ikiwahakikishia Wakenya kuwa iko tayari kusimamia uchaguzi wa mwaka 2027 kwa njia huru, ya haki na yenye kuaminika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































