#Local News

“NIKO TAYARI KUFANYA KAZI NA GACHAGUA” – SIFUNA

Ni kauli yake Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, akieleza kuwa lengo la pamoja la upinzani ni kumuondoa Rais William Ruto madarakani licha ya tofauti zao za awali za kisiasa.

Sifuna amesema vuguvugu la Linda Mwananchi liko tayari kushirikiana na mtu yeyote anayeheshimu Katiba, utawala wa sheria na anayelenga kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.

Sifuna amesisitiza uamuzi wake wa kuunga mkono hoja ya kumng’atua Gachagua ulikuwa sahihi, akidai ulihusishwa na madai ya kuingilia shughuli za Kaunti ya Nairobi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *