UCHUMI WA KENYA WAKADIRIWA KUPANDA KWA ASILIMIA 4
Uchumi wa taifa la kenya unakadiriwa kukua kwa asilimia 4.6 mwaka huu, ikitarajiwa kufuatiwa na ongezeko la zaidi ya asilimia 4.7 mwaka ujao.
Kwa mujibu wa ripoti ambayo imetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inaonyesha kuwa ingawa uchumi wa Kenya uliwahi kutarajiwa kukua kwa asilimia 5 mwaka 2025, lakini ulikwamwa kidogo kutokana na ukosefu wa utulivu ulioongezeka duniani na kupanda kwa gharama ya mafuta.
Hata hivyo,ukuaji unaokaridiwa wa uchumi wa Kenya uko nyuma ya wastani wa eneo la Afrika Mashariki wa asilimia 5.9 mwaka 2026 na asilimia 6.4 mwaka 2027, na pengo hilo kwa kiasi kikubwa linasababishwa na utendaji mzuri wa uchumi katika nchi jirani zinazokua kwa kasi zaidi.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































