TUSKER WAWANIA USHINDI WA KWANZA KAGAME CUP
Tusker wanatarajia kurejea katika njia ya ushindi watakapovaana na wenyeji Rayon Sports katika mchezo wa Kundi C wa mashindano ya CECAFA Kagame Cup utakaochezwa jijini Kigali, Rwanda
Mabingwa hao wa Kombe la Mozzartbet wanatafuta alama zao za kwanza baada ya kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wao wa ufunguzi wa mashindano hayo
Rayon Sports wanaingia katika pambano hilo wakiwa na morali ya juu baada ya kuanza kampeni yao kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ FC, matokeo yaliyowaweka kileleni mwa kundi kwa alama tatu pamoja na Al Hilal.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































