OMANYALA ASHINDWA KUNG’ARA KATIKA MBIO ZA MITA 100 MJINI GLASGOW
Ferdinand Omanyala amepoteza matumaini ya kutwaa taji lake la pili la Michezo ya Jumuiya ya Madola baada ya kumaliza katika nafasi ya sita kwenye nusu fainali ya mbio za mita 100 mjini Glasgow
Bingwa huyo wa zamani alitumia sekunde 10.19, akianza mbio kwa kasi lakini akapoteza nguvu
Mkenya mwenzake Meshack Babu pia alikosa nafasi ya kutinga fainali, hivyo kuhitimisha ushiriki wa Kenya katika mbio hizo bila mwakilishi kwenye hatua ya mwisho.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































