#Rugby #Sports

OLUKUSI AIAMINI KCB KUTAWALA MZUNGUKO WA RAGA YA WACHEZAJI SABA

Nahodha wa KCB Elvis Olukusi amesema kikosi chake kina uwezo wa kutwaa ubingwa katika kila duru ya Mzunguko wa Kitaifa wa Raga ya Wachezaji Saba baada ya kuanza vyema mashindano ya Prinsloo 7s

Olukusi amesema timu bado inahitaji kuboresha maelewano uwanjani, uimara wa safu ya ulinzi na matumizi ya nafasi za kufunga pointi, akisisitiza kuwa wachezaji wana uwezo wa kuendelea na ushindi katika duru zijazo ikiwemo Dala 7s

Nahodha huyo amesema KCB ilifika Prinsloo 7s ikiwa na azma ya kulipiza kisasi dhidi ya Strathmore Leos baada ya kupoteza dhidi yao mwaka uliopita, akieleza kuwa kikosi kimeonyesha maendeleo makubwa na kinaendelea kujiimarisha kuelekea msimu huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *