MAHAKAMA YAAMURU KUFUKULIWA KWA MWILI HOMABAY
Mahakama ya Ndhiwa imeamuru kufukuliwa kwa mwili wa Joab Otieno mwenye umri wa miaka 36 kutoka kijiji cha Kakello eneo la Seme baada ya familia yake kudai alizikwa bila idhini yao
Familia hiyo imeeleza kushangazwa na jinsi mazishi hayo yalivyofanyika wakidai kuwa mwanamke mmoja anayedaiwa kujulikana kama Jennifer Nundu alichukua mwili huo kutoka mochari bila idhini ya familia
Baba wa marehemu amesema familia haimtambui mwanamke huyo na amehoji namna alivyoweza kupata mwili na kuuzika bila kuwahusisha ndugu wa karibu huku uchunguzi zaidi ukiendelea kubaini kilichojiri.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































