TSC YAAMURIWA NA MAHAKAMA YA AJIRA KUWAFIDIA WALIMU 122 SHILINGI 100,000KILA MMOJA
Mahakama ya Ajira imeiamuru Tume ya Kuwaajiri Walimu TSC kuwalipa walimu 122 fidia ya shilingi 100,000 kila mmoja baada ya kubaini kuwa uhamisho wao kurejea Kaunti ya Mandera haukuwa wa haki na ulikiuka haki yao .
Jaji Jemimah Keli ametoa uamuzi huo kutokana na kesi iliyowasilishwa mbele yake na Chama cha Walimu katika Maeneo ya Ukame na Yenye Mazingira Magumu nchini KETHAWA dhidi ya TSC.
Walimu hao walipinga hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yao baada ya kuondoka katika vituo vyao vya kazi huko Mandera wakieleza sababu za ukosefu wa usalama kisha baadaye kuagizwa kurejea katika eneo hilo.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































