DAP-K YATAKA MGOMBEAJI WA UDA MALAVA AZUIWE
Kinara wa chama cha DAP-K Eugene Wamalwa, ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kumwondoa mgombeaji wa UDA eneo bunge la Malava David Ndakwa kwenye orodha ya wagombeaji, kwa madai kwamba Ndakwa amechochea vurugu dhidi ya mgombeaji wa DAP-K Seth Panyako.
Akizungumza mapema leo eneo hilo, Wamalwa amesema kuwa Panyako ameshambuliwa na wahuni usiku wa kuamkia leo kabla ya kufanikiwa kutoroka, akiwatuhumu maafisa wa polisi kwa kuhusika.
Wamalwa amelalamikia madai kwamba serikali inawahonga wapiga kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































