#Football #Sports

TANZANIA WAINGIA HATUA YA MWONDOANO

Timu ya Taifa Stars ya Tanzania ilivua vazi la timu ndogo katika mashindano yanayoendelea ya taifa bingwa barani Afrika AFCON 2025 baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya bao 1 dhidi ya miamba Tunisia, na kutinga awamu ya mwondoano ya mashindano hayo jana usiku.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufika awamu hiyo katika muda wa miaka 45 tangu waliposhiriki kwa mara ya kwanza.

Ismael Gharbi aliwaweka Tunisia mbele kupitia mkwaju wa penalti kabla ya mapumziko ila Feisal Salum akasawazisha kaktika kipindi cha pili.

Licha ya sare 2 na kichapo kimoja na bila ushindi wowote, Tanzania walipata haki ya kuwadhihaki Wakenya kwa ukali wa mistari ya Bongo Flavor, wakiingia awamu ya mwisho ya 16 kama mojawapo ya timu 4 zilizomaliza katika nafasi ya 3 na pointi nyingi, ikiipiku Angola kwa ubora wa mabao.

Tunisia ilimaliza ya pili katika Group C lililoongozwa na Nigeria.

Wakati uo huo, Uganda iliyaaga mashindano hayo kwa kizaazaa cha kuwatumia makipa 3 katika kipindi cha dakika 11 dhidi ya Nigeria.

Kizaazaa kilianza baada ya Salim Jamal Magoola kuingia katika nafasi ya kipa Dennis Onyango aliyejeruhiwa, ila akapata kadi nyekundu alipoushika mpira nje ya eneo lake ili kuzuia Victor Osimhen kufunga bao, nafasi yake ikichukuliwa na Nafian Alionzi.

Tanzania watamenyana na wenyeji Morocco Jumapili katika awamu ya mwondoano, siku moja baada ya Tunisia kuchua na Mali.

Nigeria watamenyana na Msumbiji.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

TANZANIA WAINGIA HATUA YA MWONDOANO

ARSENAL YATIA BREKI REKODI YA VILLA

TANZANIA WAINGIA HATUA YA MWONDOANO

SHINYALU YAENDELEA KUOMBOLEZA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *