#Local News

WAHALIFU WAWILI WAKAMATWA KISUMU

Wanaume wawili wamekamatwa Kisumu baada ya polisi kupata silaha na vitu vinavyoaminika kutumika katika shughuli za  uhalifu .

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa  x  , polisi wamesema watu hao   walikamatwa kwenye kivuko cha reli huku wakidaiwa kujiandaa kufanya uhalifu katika eneo hilo.

Operesheni hiyo ilizinduliwa baada ya wakazi kutoa tahadhari kuhusu mienendo yenye mashaka karibu na barabara yenye shughuli nyingi, na kusababisha hatua za haraka kutoka kwa maafisa waliokuwa wakishika doria.

Imetayarishwa na Jones Koikai

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *