#Football #Sports

TUDOR AAMINI ALAMA DHIDI YA LIVERPOOL MWAMKO KWA SPURS

Kaimu kocha mkuu wa Tottenham Ingor Tudor, amepongeza juhudi za wachezaji wake zilizowapa pointi moja muhimu dhidi ya bingwa mtetezi wa EPL Liverpool, na kuwapa matumaini ya kukwepa shoka la kushushwa daraja.

Bao la Richarlison katika dakika ya 90 liliwapa Spurs sare ya bao 1-1 ugani Anfield, na kutamatisha msururu wa kichapo katika mechi 6 ambao ulikuwa umeizamisha Spurs katika eneo la hatari.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Tudor, zamani akiinoa Juventus, amesema anaamini sare hiyo iliashiria mwamko mpya.

Kwa sasa wako juu ya Nottingham Forest kwa pointi 1, vita vya kujiokoa vinapochacha.

Kwa sasa Arsenal wanaongoza ligi wakiwa na pointi 70 baada ya kuandikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton, alama 9 mbele ya City walioteleza na kuandikisha sare ya pili mfululizo dhidi ya West Ham United.

Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa, Manchester United wako katika nafasi ya 3, wakilenga kumaliza katika nafasi ya 2.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *