#Football #Sports

SPURS WATENGANA NA MKUFUNZI WAO TUDOR

Klabu ya Tottenham inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, EPL, imemfuta kazi kocha wake Igor Tudor, baada ya mechi 7 pekee klabu hiyo inapopambana kuepuka kushushwa daraja.

Chini ya uongozi wake, Spurs walipoteza mechi 5 na kuachwa nje yak inyanng’anyiro cha kuwania kombe la klabu bingwa bara Ulaya, na sasa wana pointi moja pekee nje ya eneo la kushushwa daraja.

Kupitia taarifa, Spurs imesema Tudor ameondoka kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.

Tudor hakuwahutubia wanahabari baada ya kichapo cha mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Nottingham Forest, baada ya kupata taarifa mwishoni mwa mechi hiyo kuhusu kifo cha babake.

Raia huyo wa Croatia aliteuliwa mwezi jana kuchukua nafasi ya Thomas Frank, ila akashindwa kutia breki gari la kuelekea ligi ya Championships kwa Spurs.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SPURS WATENGANA NA MKUFUNZI WAO TUDOR

WAKENYA WAWIKA BERLIN

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *