#Local News

UJUMBE WA RUTO KUHUSU PASAKA

Huku Wakristo kote ulimwenguni wakiadhimisha siku kuu ya Pasaka, Rais William Ruto amewatakia Pasaka njema huku akiwahimiza kuitumia kutafakari kuhusu mwanzo mpya maishani mwao.

Kupitia kanda fupi ya video aliyoichapisha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii, Ruto amesema kipindi cha Pasaka ni mwanzo mpya miongoni mwa familia za wakenya na kuwataka kuliombea taifa.

Amewataka kuzingatia mafundisho muhimu ya Yesu kuhusu upendo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *