#Local News

MVUA KUBWA YAENDELEA KUSHUHUDIWA TRANS NZOIA

Wakazi wa wadi ya Kiptoro- Chepsiro kaunti ya Trans Nzoia wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na ongezeko la watu kufa maji eneo hilo, watu wawili wakiripotiwa kufariki katika muda wa wiki moja iliyopita.

Naibu chifu wa Kiboswa Gilbert Chepsiror, amesema kisa cha hivi punde kinamhusisha mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo, aliyeripotiwa kujirusha katika mto Moiben unaounganisha kaunti hiyo na Uasin Gishu.

Amewahimiza wakazi kusaka ushauri nasaha wanaposongwa na mawazo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *