#Local News

DAKTARI GIKONYO AHOJIWA MAHAKAMANI KATIKA  KESI YA GACHAGUA

Kesi ya kusikizwa kuondolewa Mamlakani aliyekuwa Naib Rais Rigadhi Gachagua inasikizwa Mahakamani

Daktari wa magonjwa ya moyo Daniel GiKonyo  amedhibitisha kupokea simu kutoka kwa Rais William Ruto aliyetaka kujua hali ya kiafya ya aliyekuwa Naib Rais Rigadhi Gachagua baada ya kukimbizwa hospitalini wakati wa kusikizwa kwa hoja ya kumung’atua ofisini  katika  bunge la seneti.

Akizungumza katika mahakama Gikonyo  amaeeleza kuwa ni jukumu lake kusema ukweli akikiri kumweleza Rais kuwa  bado alikua anafanya vipimo,kulingana na  Gikonyo  baadae alimuomba  Gachagua ruhusa ya  kueka wazi kwa umma tatizo lililokuwa limemkumba wakati huo kabla ya kutotaarifu umma kuhusu hali ya afya yake.

Daktari Gikonyo amefika kuhojiwa kuhusiana na kiapo alichoapa kuhus ushaidi wake katika siku ya mwisho ya vikao hivyo kabla ya majaji wanaosikiza kesi hiyo kutangaza siku ambayo watatangaza uwamuzi  wa kesi hiyo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *